UMUHIMU WA KUTUNZA KUMBUKUMBU, KWENYE MRADI WAKO WA KUKU

1. TAARIFA ZA MANUNUZI ZITAFAHAMIKA.

Mradi wowote wa kuku, ni lazima uhusishe manunuzi ya bidhaa tofauti tofauti, kama madawa, chanjo, vifaa kama Drinkers na feeders, pamoja na vifaranga. Taarifa hizi zinapaswa kuandikwa na jumla ya gharama zake, kufahamika kwenye daftari au card ya kutunzia kumbukumbu.

 

AMSTERDAM KUKU_20260427_061906_0000

2. TAARIFA ZA MAENDELEO YA KUKU.

Taarifa hizi, zitajumuisha idadi ya kuku wagonjwa, na idadi ya vifo vitakavyotokea wakati mradi ukiendelea, taarifa hizi zitajumuishwa kila siku na kupata taarifa ya jumla kila wanapofunga week.

 

3. TAARIFA ZA UTAGAJI WA MAYAI.

Ufugaji wenye tija wa kuku, wa mayai ni lazima mfugaji awe na tamaduni ya kuandika idadi ya mayai yakiyotagwa kila siku, idadi ya mayai yaliyopasuka wakati wa uokotaji, pamoja na mayai yenye changamoto tofauti tofauti.mfano crack, wrinkled egg shell.

 

4. TAARIFA ZA HALI YA HEWA NDANI NMYA BANDA.

Kwa kuzingatia matumizi sahihi ya vifaa vya kisasa kama HTC 1( Temperature & humidity sensor) mfugaji ataweza kutunza taarifa za joto la Banda na hali ya unyevu unyevu bandani, ili kulinganisha na mahitaji ya kuku husika Kwa kuzingatia umri wao.

 

5. TAARIFA ZA MAUZO YA KUKU, MAYAI, NYAMA NA MBOLEA.

Kwa kuzingatia aina ya mradi wa kuku, taarifa za mauzo ndio msingi wa maendeleo ya mradi wowote wa kuku, hapa ndipo mfugaji atapata kujua bei ya mazao yake kama nyama na mayai, kiwango Cha faida na bei elekezj iliyopo sokoni, na mwisho kujua kama mradi umeingiza faida ya hasara.

Scroll to Top